Wafungwa alfu saba waachiliwa huru

Na Beatrice Maganga

Rais Uhuru Kenyatta ametimiza ahadi yake ya kupunguza msongamano katika magereza ya humu nchini ili kisiwapo kisingizio cha kutohukumiwa kwa wahusika wakuu wa ufisadi kwa madai ya kukosekana kwa nafasi za kuwazuilia. Rais ametangaza kuachiliwa huru kwa wafungwa elfu saba waliohukumiwa kwa makosa madogo madogo na waliokuwa karibu kukamilisha vifungo vyao.

Rais amemtaka Jaji Mkuu mpya, David Maraga kuhakikisha kesi hasa za ufisadi zinaharakishwa ili kuwapa wananchi imani katika vita dhidi ya ufisadi.

Wiki hii, Rais alizisuta idara mbalimbali za serikali ikiwamo Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma na idara ya mahakama kwa kutowajibikia suala la ufisadi. Vilevile alisema sheria inamzuia kuwachukulia hatua wahusika wa uhalifu huo.