Conselus Kipruto kushiriki mbio za mita 3k kuruka maji na viunzi saa kumi na mbili jioni

Na,Hassan Ali

Matumaini ya Wakenya kutwaa medali leo hii yamo mikononi mwa washiriki wa mbio za mita 3k kuruka maji na viunzi. Fainali hiyo itaandaliwa saa kumi na mbili bado dakika kumi jioni. Kenya inawakilishwa katika mashindano hayo na Conselus Kipruto, bingwa wa medali ya dhahabu mashindano ya olimpiki huko Beijing Uchina mwaka 2008 Brimin Kipruto na Baba Yao bingwa mtetezi wa mbio hizo, aliyetwaa medali mashindano ya olimpiki mwaka 2012 Ezekiel Kembo. Kila la kheri Team Kenya.