KNUT Yapigasaini Mkataba wa Makubaliano ya Utendakazi na TSC

Katika juhudi za kukomesha migogoro ya mara kwa mara inayokumba sekta ya elimu, Chama cha Walimu Nchini, KNUT kimesaini mkataba wa makubaliano ya utendakazi na Tume ya Huduma kwa Walimu, TSC. Mwenyekiti wa KNUT Mudzo Nzili, katibu wake Wilson Sossion, viongozi wa TSC akiwamo mwenyekiti Profesa Lydia Nzomo na afisa Mtendaji, Nancy Macharia wametia saini mkataba huo wa makubaliano.

Kwa mujibu wa viongozi hao, mkataba huo mbali na mambo mengine utaimarisha nidhamu katika sekta ya elimu na kushughulikia masuala ya mishahara na marupurupu ya walimu.

Aidha Katibu Mkuu wa KNUT Willson Sossion amegusia suala la mwongozo wa maadili akisema kwa sasa tume hiyo inapitia kielelezo hicho kabla ya kutoa mwelekeo.


Hata hivyo amewashauri walimu kuwa watulivu na kusema suala la walimu kutangaza mali wanazomiliki ni la kisheria na halifai kuwatia hofu.

Na, Kelvin Karani/Sulleiman Yeri

Related Topics

KNUT TSC